IQNA

Azerbaijan yaandaa kikao cha ‘Mtandao wa Wafanyabiashara wa OIC’

16:50 - November 23, 2011
Habari ID: 2227599
Kikao cha kwanza cha Jukwaa la Mtandao wa Wafanyabiashara Vijana kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kimeanza katika mji mkuu wa Azerbaijan, Baku.
Ujumbe wa Katibu Mkuu wa OIC Profesa Ekmeleddin Ihsanoglu ulisomwa katika sherehe za ufunguzi Jumanne 22 Novemba.
Aidha katika hafla hiyo wametunukiwa zawadi vijana 10 wa Kiislamu ambao wamekuwa na nafasi kubwa katika kuleta mabadiliko duniani. Lengo la zawadi hizo limetajwa kuwa ni kuwapa motisha vijana Waislamu wanaofanya biashara katika nchi za OIC.
Waliopewa zawadi hizo wana umri wa chini ya miaka 30 na wamekuwa na nafasi kubwa katika uga wa biashara, sanaa, michezo na kulinda mazingira.
Kongamano hilo la siku mbili limewaleta pamoja vijana 150 kutoka nchi mbalimbali wanachama wa OIC.
903776
captcha