IQNA

Matukio ya kimapinduzi Misri

16:44 - November 23, 2011
Habari ID: 2227613
Wamisri wenye hasira wanaolalamikia mwendo wa kinyonga wa kukabidhi madaraka ya nchi kwa serikali ya kiraia wameendelea kusalia katika mitaa ya Cairo na kwenye miji mingine ya Misri wakiendeleza maandamano yao, licha ya maridhiano yaliyopendekezwa na Baraza Kuu la kijeshi la nchi hiyo.
Vilevile kujiuzulu serikali ya Essam Sharaf Waziri Mkuu wa muda wa Misri kunathibitisha kuwa wananchi ndio wenye uwezo wa kuchukua maamuzi kuhusu mustakbali wa nchi hiyo. Weledi wengi wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa, kujizulu serikali ya muda ya Misri ni hatua ya kwanza ya kurudi nyuma wanajeshi watawala wa nchi hiyo mbele ya matakwa ya wananchi. Serikali ya muda wa Misri iliteuliwa kwa usimamizi wa moja kwa moja wa Baraza Kuu la Kijeshi la nchi hiyo na si kwa mujibu wa matakwa ya Wamisri.
Matukio ya sasa nchini Misri yanaonyesha namna irada ya wananchi ilivyo na nguvu zaidi kuliko watawala wa kijeshi wa nchi hiyo. Vilevile kujiuzulu serikali ya Essam Sharaf Waziri Mkuu wa muda wa Misri kunathibitisha kuwa wananchi ndio wenye uwezo wa kuchukua maamuzi kuhusu mustakbali wa nchi hiyo. Weledi wengi wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa, kujizulu serikali ya muda ya Misri ni hatua ya kwanza ya kurudi nyuma wanajeshi watawala wa nchi hiyo mbele ya matakwa ya wananchi. Serikali ya muda wa Misri iliteuliwa kwa usimamizi wa moja kwa moja wa Baraza Kuu la Kijeshi la nchi hiyo na si kwa mujibu wa matakwa ya Wamisri.
Ukweli wa mambo ni kuwa, serikali ya Essam Sharaf ilikuwa serikali iliyoteuliwa na wanajeshi na kwa msingi huo wananchi wa Misri waliitambua serikali hiyo ya muda kuwa mtekelezaji wa maagizo yanayotolewa na Baraza Kuu la Kijeshi la nchi hiyo. Baraza hilo ambalo lilichukua mamlaka ya kuiongoza Misri mwezi Februari sambamba na kuenguliwa madarakani utawala wa Hosni Mubarak, liliteuliwa na dikteta huyo wa zamani wa Misri. Hatua hiyo pamoja na upuuzaji wa wanajeshi hao watawala kwa matakwa ya wananchi na malengo ya mapinduzi makubwa yaliyojiri huko Misri, vimewafanya wananchi waamini kuwa, hali ya mambo ya Misri haijabadilika licha ya mapinduzi yaliyofanyika nchini humo. Hii ni kwa sababu, watawala walioko madarakani huko ni watu walioteuliwa na utawala wa zamani wa Misri.
Aidha hatua ya Baraza Kuu la Kijeshi la Misri ya kutowashughulikia viongozi mafisadi wa utawala wa zamani imewafanya wananchi wa Misri wakose imani na wanajeshi walioko madarakani. Swali linaloulizwa na wananchi wa Misri hivi sasa ni kwamba, uongozi wa sasa una tofauti gani na zama za utawala wa dikteta Mubarak? Fikra hiyo imetokana na utendaji mbaya wa wanajeshi walioko madarakani.
Hakuna shaka kuwa, jeshi au kwa ibara nyingine wanajeshi ambao kwa miaka kadhaa wamekuwa mhimili mkuu wa mfumo wa kisasia wa Misri, hawataki kupoteza ushawishi wao katika kipindi cha baada ya mapinduzi. Suala hilo linaonekana wazi katika rasimu ya katiba mpya ya Misri iliyotayarishwa chini ya uongozi wa wanajeshi hao. Katika rasimu hiyo jeshi la Misri limepewa nafasi na mamlaka makubwa zaidi ya Serikali na Bunge.
Zaidi ya hayo ni kuwa, mwenendo wa Baraza Kuu la Kijeshi la Misri wa kutowachukulia hatua viongozi na wawakilishi wa ngazi ya juu wa chama cha Demokrasia ya Taifa, chama tawala cha zamani cha Misri, na kuwarejesha baadhi ya viongozi wa chama hicho katika medani ya siasa ya nchi hiyo, yote hayo yanaimarisha dhana kwamba, watu walio karibu na utawala wa Hosni Mubarak wanashirikiana na wanajeshi watawala wa Misri. Hasa ikizingatiwa kuwa, katika kipindi cha miezi minne ya hivi karibuni watawala hao wa kijeshi wameonyesha kuwa hawana nia ya kuondoka katika uwanja wa saisa na kurejea makambini. Hii ni katika hali ambayo, kukabidhiwa madaraka kwa serikali ya kiraia na iliyochaguliwa kidemokrasia ilikuwa moja ya kaulimbiu kuu za wananchi wa Misri baada ya ushindi wa mapinduzi.
903730
captcha