Kwa mujibu wa wa mwandishi wa IQNA, Tawi la Afrika, katika mkutano uliofanyika wiki hii Pretoria na kuhudhuriwa na wakurugenzi wa vituo vya Mashia , suala la kushirikiana katika hafla za Muharram lilijadiliwa.
Washiriki katika mkutano huo walitoka katika miji yenye Mashia wengi kama vile Pretoria, Johannesburg, Karangua, Durban, Cape Town, Gautama na Soweto.
Halfa hizo ni za kuomboleza tukio la kusikitisha la kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS na wafuasi wake watiifu 72 katika jangwa la Karbala tarehe 10 Muharram mwaka 61 Hijria.
Idadi ya Waislamu Afrika Kusini inakadiriwa kuwa milioni moja au asilimi 2 ya watu wa Afrika Kusini.
903382