IQNA

Hamas yalaani uharibifu wa msikiti al-Akhalil

16:42 - November 26, 2011
Habari ID: 2229192
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imelaani vikali hatua ya askari wa utawala haramu wa Israel ya kubomoa na kuharibu msikiti wa Yata katika mojawapo ya viunga vya mji wa al-Khalil.
Kwa mujibu wa tovuti ya CPI, harakati ya Hamas, imetoa taarifa ikilaani vikali hatua hiyo ya kichokozi ya askari wa utawala wa Kizayuni ambayo imeandamana na vitendo vingine vya kukashifu na kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu.
Sehemu moja ya taarifa hiyo inasema kuwa utawala haramu wa Israel umechukua hatua ya kuharibu msikiti huo kama mojawapo ya njia za kudhoofisha moyo wa mapambano wa wananchi wa Palestina. Imesema lengo jingine ni kutaka kupora mali na ardhi za Wapalestina pamoja na kutoa mashinikizo dhidi yao.
Taarifa hiyo inasema kwamba licha ya kuwa utawala haramu wa Israel unadumisha ukandamizaji huo kwa madhumuni ya kuongeza maradufu kasi ya ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina, lakini kamwe hawatoacha mapambano yao ya kukabiliana na ukandamizaji huo.
Taarifa ya Hamas imezitaka nchi za Kiarabu zichukue msimamo madhubuti kuhusiana na ujenzi wa vitongoji hivyo pamoja na jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina.
Utawala huo siku ya Alkhamisi ulishambulia na kuharibu Msikiti wa Yata na kisha akaharibu mashamba na mabustani ya Wapalestina katika maeneo ya karibu. 905113
captcha