IQNA

Kikao cha 'Ijumaa ya Kuunga Mkono Masjidul Aqsa chafanyika Misri

17:00 - November 27, 2011
Habari ID: 2229955
Kikao cha 'Ijumaa ya Kuunga Mkono Masjidul Aqsa' kilifanyika siku ya Ijumaa katika Msikiti Mkuu wa al-Azhar mjini Cairo, mji mkuu wa Misri. Kwa mujibu wa tovuti ya CPI kikao hicho kilihudhuriwa na zaidi ya wanafikra, wasomi, wahadhiri na wanazuoni 5000.
Kikao hicho ambacho pia kilihudhuriwa na wabunge na viongozi wa makundi na vyama vya kisiasa na kijamii kilikuwa na lengo la kulaani ujenzi wa vitongoji vya Mayahudi na kufutwa alama na athari za kihistoria za Waarabu na Waislamu katika mji wa Quds.
Katika hotuba yake kwa washiriki wa kikao hicho, Ahmad Tayyib, Sheikh wa al-Azhar amesema kuwa mji wa Quds Tukufu ni mstari mwekundu wa Waislamu na kwamba kwa msingi huo hakuna mtu yoyote anayepasa kuuvuka. Amesema nchi zote za Kiislamu zinapasa kufanya juhudi za kuvunja njama za utawala wa Kizayuni za kuufanya mji huo mtakatifu kuwa wa Kiyahudi. Wakati huohuo, Abu ar-Rahman al-Birr, mwanachama wa Harakati ya Ikhwanul Muslimeen amewataka Waislamu wote duniani kuchukua hatua za dharura kwa lengo la kuvunja njama za kuufanya mji huo kuwa wa Kiyahudi na vilevile kusimamisha mara moja uharibifu unaofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya athari za Kiislamu na Kiarabu katika mji huo.
Khalil al-Hayya, mwanachama wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Hamas ameshukuru juhudi za Sheikh wa al-Azhar za kuandaa kikao cha kuunga mkono Masjidul Aqsa na kuwataka wapigania haki wote duniani kuunga mkono Quds Tukufu. Amewataka Waarabu kuungana kwa ajili ya kukomboa Quds kutoka mikononi mwa maghasibu wa Kizayuni. 905414
captcha