IQNA

Katibu Mkuu wa OIC alaani hujuma ya NATO Pakistan

16:17 - November 29, 2011
Habari ID: 2231129
katibu Mkuu wa Jumuiya ya ushirikiano wa Kiislamu (OIC) Ekmeleddin Ihsanoglu amelaani vikali hujuma iliyofanywa hivi karibuni na vikosi vya Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi NATO iliyoua wanajeshi 24 wa Pakistan.
Katika salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga na serikali ya Pakistan, Ihsanoglu amesema mashambulio hayo ni ukiukaji mkubwa wa utawala wa Pakistan na ni jambo lilisokubalika.
Ameihakikishia Pakistan kuwa OIC itaendeleza ushirikiano wake na nchi hiyo na kusema kuwa hatua zichukuliwe kuzuia hujuma kama hizo.
Ihsanoglu ameitaka NATO kuzuia hatua zozote ambazo zitavuruga zaidi hali mbaya ya usalama katika eneo hilo.
907261
captcha