IQNA

Umati mkubwa wa waombolezaji wamiminika Karbala

12:21 - November 30, 2011
Habari ID: 2231843
Umati mkubwa wa wapenzi na wafuasi wa Imam Hussein (as), mjukuu wa Mtume Mtukufu (saw), wamekuwa wakishiriki kwa wingi katika maombolezo ya kumbukumbu ya kifo cha mtukufu huyo katika Haram yake huko katika mji mtakatifu wa Karbala.
Tokea mwanzoni mwa mwezi huu wa majonzi na huzuni wa Muharram umati mkubwa wa waombolezaji umekuwa ukishiriki katika marasimu tofauti za kuomboleza kifo cha Imam Hussein aliyeuawa na maadui wa Uislamu wakiongozwa na Yazid bin Muawiyya.
Maduka na masoko ya mji huo pia yamefungwa tokea mwanzoni mwa mwezi huu wa Muharram kwa mnasaba huohuo na bendera nyeusi zinapeperushwa katika sehemu hizo kama ishara ya kuheshimu maombolezo hayo. Maombolezo yanafanyika katika sehemu hizo katika kipindi chote cha siku kumi za mwanzoni mwa mwezi huu badala ya shughuli za kawaida za kibiashara.
Idara ya Haram ya Imam Hussein (as) imekuwa ikitoa suhula maalumu kwa wafanyaziara na waombolezaji wa mtukufu huyo na pia vyombo vya usalama vya mji mtakatifu wa Karbala vimeimarisha usalama kwa ajili ya kulinda maisha ya waombolezaji katika siku hizi muhimu. 907958
captcha