IQNA

Maonyesho ya Kimataifa wa Bidhaa Halali kufanyika Moscow

16:15 - November 30, 2011
Habari ID: 2232160
Baraza la Mamufti wa Russia limetangaza kuwa litaandaa Maonyesho ya Tatu ya Kimataifa ya Bidhaa Halali mjini Moscow Juni 7-10 mwaka 2012.
Maonyesho hayo yanalenga kuangazia uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma halali duniani. Aidha maonyesho hayo yatakuwa fursa ya kuchangia ustawi wa biashara ya Kiislamu na uzingatiwaji maadili katika uzalishaji.
Pembizoni mwa maonyesho hayo pia kutakuwa na mkutano kuhusu mfumo wa kifedha wa Kiislamu na uimarishwaji uhusiano wa kibiashara kati ya Russia na nchi za Kiislamu. Suala la kutoa vyeti vya bidhaa Halali pia linatazamiwa kujadiliwa. Zaidi ya mashirika 150 katika sekta ya ‘Halal’ kutoka maeneo mbalimbali ya Russia pamoja na Malaysia, Iran, Uturuki, Uingereza, Pakistan , Saudi Arabia, Indonesia n.k yatashiriki katika maonyesho hayo.
Maonyesho ya Halal Moscow pia yatakuwa na programu za kiutamaduni kuhusu chakula cha Waislamu wa Russia. Vilevile kutakuwa na maonyesho ya mavazi ya Kiislamu pamoja na mashindano ya kuchora na upakaji hina.
908647
captcha