IQNA

Iran kufungua madrasa 20000 mpya za Qur’ani

16:19 - November 30, 2011
Habari ID: 2232174
Mshauri wa Masuala ya Qur’ani katika Wizara ya Elimu nchini Iran ametangaza mpango wa kufunguliwa madrasa 20,000 mpya za Qur’ani kote nchini katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.
Akizungumza na IQNA, Mohammad Bonyadi amesema tayari baadhi ya madrasa hizo zimeshafunguliwa lakini hazijazinduliwa rasmi hadi zifikie viwango vinavyohitajika.
Amesema suala la viwango bora katika madrasa za Qur’ani linapewa kipaumbele. Ameongeza kuwa mwaka jana madrasa 10,000 za Qur’ani zilifunguliwa nchini katika mpango wa Hati ya Kustawisha Utamaduni wa Qur’ani na katika fremu ya muongozo wa Tume ya Elimu ya Qur’ani.
Amesema kwa ujumla vyuo 50,000 vya Qur’ani vitafunguliwa kote Iran katika kipindi cha miaka michache ijayo. Ameongeza kuwa kuna walimu 185,000 wa Qur’ani waliohitimu ambayo wanatoa mafunzo katika madrasa za Qur’ani nchini Iran.
Afisa huyo wa Wizara ya Elimu ya Iran amesema viitabu maalumu vinavyotumiwa na wanafunzi wanaosoma Qur'ani vimechapishwa na kusambazwa katika shule kote nchini.
907900
captcha