Kwa mujibu wa tovuti ya mcetv.fr wanafunzi ya shule ya Kiislamu ya Vauquelin katika mji uliotajwa walipigwa na butwaa baada ya kuona maandishi hayo ya kashfa na uvunjiwaji heshima matukufu ya Kiislamu yakiwa yameandikwa kwenye kuta za shule yao walipokuwa wakiingia kwenye kituo hicho cha masomo kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za kawaida.
Licha ya kuchora alama za msalaba na nembo za manazi wa Ujerumani kwenye kuta za shule hiyo maadui hao wa Uislamu pia waliandika kwa rangi nyekundu nara za chuki kama vile 'wafukuzeni Waislamu Ufaransa' na 'Uislamu unapasa kuondolewa Ufaransa' kwenye kuta hizo.
Bila kupoteza wakati, wakuu wa elimu wa Ufaransa walitoa taarifa wakilaani kitendo hicho na kusema kwamba mashambulio ya makundi ya ubaguzi wa rangi katika vituo vya masomo vya nchi hiyo ni jambo lisilokubalika kabisa. Wamevitaka vyombo vya usalama kufuatilia na kuwatia nguvuni wahusika wa kitendo hicho cha kibaguzi dhidi ya Waislamu wa Ufaransa. 908426