Kituo kilifunguliwa mapema mwaka huu, limeripoti Shirika la Habari la Rasid.
Kituo hicho kilifungwa siku ya Jumanne, Novemba 29 baada ya kuanza hafla za Muharram za kuomboleza kuuawa shahidi Imam Hussein AS.
Mwanazuoni mwandamizi wa Kishia Sheikh Ali Ad-Dahnin ambaye ni mkosoaji mkali wa utawala wa kifalme Saudia alikuwa akitoa hotuba katika kituo hicho kila siku.
Kufungua kituo hicho ni hatua nyingine inayoashiria kukandamizwa Mashia waliowengi katika eneo hilo la Saudia.
Askari usalama wa Saudi Arabia wamesambazwa kwa wingi katika mitaa ya mji wenye Waislamu wengi wa madhehebu ya Shia wa Qatif huko mashariki mwa nchi hiyo kwa kisingizio cha kulinda amani.
Mashirika ya kutetea haki za binaadamu kama vile Amnesty International yameukosoa vikali utawala wa Saudia kwa kuwakandamiza wananchi wa Qatif. Ufalme wa Saudia unaopata himaya kamili kutoka Marekani na nchi za Magharibi umechukua hatua kukandamiza mwamako wa Kiislamu nchini humo kwa kuhofia kupata hatima kama ile iliyowapata vibaraka wa Marekani huko Afrika Kaskazini. 908432