IQNA

Uingereza inataka kulifanya Baraza la Usalama lipoteze itibari yake

13:59 - December 03, 2011
Habari ID: 2233192
Khatibu wa sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuwa Baraza la Usalama na nchi za Ulaya zinataka kupoteza heshima yao kutokana na njama za Uingereza.
Huku akishiria msimamo wa hivi karibuni wa serikali ya Uingereza dhidi ya Iran, Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami, Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya jana mjini Tehran aliongeza kuwa, njama za serikali ya London zimefichuka katika nchi za ulimwengu wa Kiislamu na ni kwa sababu hiyo ndio maana London inataka kufidia suala hilo kwa kutumia nchi nyingine za Ulaya na Umoja wa Mataifa.
Ayatullah Khatami aidha amesisitiza kuwa, serikali ya Uingereza mara kadhaa imeshindwa na taifa la Iran, na miongoni mwa masuala yanayothibitisha hilo ni kupitishwa mswada wa hivi karibuni na Bunge la Iran wa kupunguza uhusiano na nchi hiyo.
Aidha amesema Siku ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu yaani Disemba 7 ni nembo ya mapambano ya wanafunzi dhidi ya ubeberu katika kukabiliana na Marekani na Uingereza na amesisitiza kuwa kuuawa shahidi wanafunzi kadhaa katika siku hiyo mwaka 1953 ni ushahidi wa kujivunia wa wanafunzi wa Iran.909431
captcha