IQNA

Sisitizo la kulindwa umoja wa Pakistan katika siku za Muharram

16:56 - December 03, 2011
Habari ID: 2233465
Washiriki wa kikao kilichofanyika jana Ijumaa katika mji wa Rawalpindi huko Pakistan kuhusiana na maombolezo ya mwezi mtukufu na wa huzuni wa Muharram wamesisitiza umuhimu wa kulindwa umoja na mshikamano wa Kiislamu na kitaifa wa Wapakistan katika siku hizi muhimu za kukumbuka mauaji ya mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) Imam Hussein (as).
Kwa mujibu wa gazeti la Pakistan Observer, washiriki wa kikao hicho wamesisitiza kwamba Waislamu wanapasa kuimarisha moyo wa udugu na umoja baina yao katika siku hizi za huzuni.
Katika kikao hicho kilichoshirikisha idadi kubwa ya shakhsia wa Kisuni na Kishia, Pir Muhammad Naqib Rahman, mmoja wa shakhsia muhimu wa kidini nchini Pakistan amesema kwamba tukio la Karbala na mapambano ya Imam Hussein (as) na wafuasia wake watiifu yanahuisha utukufu wa Kiislamu.
Amesema moyo wa kijitolea wa mashahidi wa Karbala daima utaendelea kuwapa moyo na azma ya mapambano watu wema duniani kwa lengo la kuhuisha utukufu na adhama ya Kiislamu ulimwenguni. 909635
captcha