Kituo cha habari cha Aswatul Iraq kimemnukuu Meja Jenerali Alaa al Ghanimi akisema kuwa askari usalama wamejizatiti katikati na katika maeneo ya kuingia mjini Karbala katika siku hizi za kabla ya Ashura (tarehe kumi Muharram) ili kulinda usalama wa wafanyaziara katika mji huo.
Alaa al Ghanimi ameongeza kuwa idadi ya Waislamu wanaokwenda kumzuru Imam Hussein (as) inaongezeka zaidi kadiri siku ya Ashura inavyokaribia. Amesema kuwa kuongezeka idadi ya wafanyaziara kunazidisha haja ya kuwepo mipango maalumu ya kiusalama ikiwa ni pamoja na kuzidishwa idadi ya askari usalama katika mji wa Karbala kwa lengo la kudhibiti hali ya mambo mjini humo.
Meja Jenerali al Ghanimi amesema kuzidishwa idadi ya askari usalama mjini Karbala kunawapa hali ya utulivu watu wanaokwenda katika mji huo kwa ajili ya kufanya ziara.
Msemaji wa polisi ya Karbala amesema mbali na vituo vya upekuzi katika milango ya kuingilia katika mji huo, vyombo vya usalama vinatumia mitambo ya kisasa ya kudhibiti maeneo mbalimbali ya mji huo. 910093