Msikiti huo uliopewa jina la al Rahman ulifunguliwa katika sherehe zilizohudhuriwa na wawakilishi wa nchi 40.
Msikiti huo umejengwa katika ardhi yenye ukubwa wa mita mraba 3300 na una uwezo wa kupokea zaidi ya watu elfu tatu wanaokwenda kutekeleza ibada ya Swala. Msikiti huo una mirana yenye urefu wa mita 27.
Ujenzi wa Msikiti wa al Rahman ulianza mwaka 1994 kwa kutumia misaada ya wananchi lakini ulichelewa kwa sababu mbalimbali na hatimaye umefunguliwa wiki hii.
Kabla ya kufunguliwa msikiti huo, Waislamu wa mji wa Kiev walikuwa wakitekeleza ibada ya Swala na shughuli nyingine za kidini katika Kituo cha Kiislamu cha mji huo na wakati mwingine walikuwa wakilazimika kuswalia nje kutokana na udogo wa eneo hilo. 909782