IQNA

Iran yalaani ukatili wa jeshi la Yemen na kimya cha kimataifa

14:51 - December 04, 2011
Habari ID: 2233892
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali hatua ya serikali ya Yemen kukandamiza kinyama wananchi Waislamu wanaoandamana kupinga dhulma na udikteta.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Ramin Mehmanparast ameikosoa jamii ya kimataifa kwa kunyamazia kimya jinai za dikteta Ali Abdullah Saleh dhidi wananchi wa Yemen. Mehmanparast amesisitiza kuwa suluhisho lolote la mgogoro wa Yemen linapaswa kuzingatia matakwa halali ya wananachi. Ameongeza kuwa Iran inalaani uingiliaji wa kigeni katika masuala ya Yemen na ametoa wito kwa vyama, makundi, makabila na wasomi wa Yemeni kuwa macho.
Mamia ya watu wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa nchini Yemen tokea ianze harakati ya mapambano ya wananchi dhidi ya dikteta Saleh anayepata uungaji mkono mkubwa kutoka Marekani na Saudi Arabia.
910408
captcha