IQNA

Mahafidhi wa Qur'ani wa Haram ya Imam Hussein washiriki katika maombolezo ya Ashura

18:02 - December 07, 2011
Habari ID: 2235016
Mahafidhi wa Darul Qur'ani ya Haram ya Imam Hussein (as) katika mji mtakatifu wa Karbala jana walishiriki katika shughuli ya kuomboleza mauaji ya mjukuu huyo wa Mtume Muhammad (saw).
Mahafidhi hao walishiriki katika shughuli za maombolezo katika msafara ulioanzia kwenye Haram ya Abul Fadhl Abbas hadi kwenye Haram ya Imam Hussein (as).
Katika kipindi chote cha maombolezo hayo mahafidhi hao walikariri nara kuhusu harakati ya mapambano ya Imam Hussein (as) na mafundisho ya Qur'ani Tukufu huku wakiwa wamebeba nakala za kitabu hicho na bendera zenye rangi nyeusi.
Mahudhurio makubwa ya makari na mahafidhi wa Qur'ani Tukufu wa Darul Qur'an katika maombolezo ya siku ya Ashura yamefanyika kwa mpangilio maalumu na kuwavutia watu wengi waliokwenda kwenye Haram ya Imam Hussein kwa ajili ya ziara.
Kundi hilo la mahafidhi wa Qur'ani Tukufu la Haram ya Imam Hussein (as) lilianzishwa miaka mitatu iliyopita kwa shabaha ya kuwahamasisha makari wa Qur'ani kushiriki kwa wingi katika marasimu na maombolezo ya kukumbuka tukio la kuuawa Bwana wa Mashahidi Imam Hussein bin Ali (as). 911801

captcha