Tume ya Uchaguzi ya Misri leo jioni imetangaza matokeo ya mwisho ya awamu ya pili ya uchaguzi wa Bunge nchini humo, uliofanyika kwenye mikoa 9 na kusema kuwa, Chama cha Uhuru na Uadilifu ambacho ni tawi la kisiasa la kundi la Ikhwanul Muslimin kimefanikiwa kupata ushindi mkubwa wa asilimia 62 ya viti vilivyowaniwa.
Vyama vingine vilivyoshiriki kwenye awamu hii ya pili ya uchaguzi huo ni kile cha kisalafi cha an Nur kilichopata viti 5, na wagombea binafsi ambao wamepata viti 7.
Kundi la Ikhwanul Muslimin lilipata ushindi mkubwa pia katika awamu ya kwanza ya uchaguzi huo wa kihistoria.
Awamu nyingine za uchaguzi huo zitafanyika katika siku za usoni na tayari imetabiriwa kuwa, wanaharakati wa Kiislamu wataendelea kupata ushindi katika awamu hizo pia.
911423