IQNA

Ensaiklopidia ya Tiba ya Kiislamu yachapishwa Iran

23:49 - December 07, 2011
Habari ID: 2235038
Ensaiklopidia kubwa zaidi ya tiba ya Kiislamu imechapishwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na itaanza kusambazwa nchini Jumamosi Disemba 10.
Ensaiklopidia hiyo ilitayarishwa na marehemu Ayatullah Mostafa Noorani na imechapishwa na Shirika la Uchapishaji la Ekram.
Naseer Muhammadi Fard mkurugenzi wa uchapishaji wa shirika la Ekram amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa Ensaiklopidia hiyo ina juzuu tisa na kwamba chapa ya kwanza ina nuskha 5000.
Ensaiklopidia hiyo itauzwa kwa 120 US$ hapa Iran.
Ensaiklopidia hiyo huko nyuma iliwahi kuchapishwa hadi juzuu ya nne na ilipongezwa sana na wanazuoni wa Kiislamu na wanasayansi kutoka nchi mbalimbali duniani.
911579

captcha