Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu Ekmeleddin Ihsanoglu amelaani uamuzi huo na kusema kuwa siasa hizo za kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi ya Quds huko Palestina zinafanyika kwa lengo la kutenganisha mji huo wa Kiislamu na ardhi za Palestina na kubadili muundo wa jamii ya eneo hilo. Amesisitiza kuwa vitendo hivyo vinakiuka sheria za kimataifa.
Ihsanoglu ameutaka Umoja wa Mataifa na Kamati ya Pande Nne kwa ajili ya amani ya Mashariki ya Kati kutekeleza majukumu yao kuhusu Quds na kukomesha vitendo vinavyokiuka sheria vya Israel kwa kuchukua misimamo madhubuti.
Taarifa hiyo ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu imetolewa baada ya kamati ya ujenzi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuafiki ujenzi wa nyumba mpya 650 za walowezi wa Kiyahudi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina. 910609