IQNA

Toleo jipya la Jarida la Sayansi na Teknolojia la ISESCO

15:58 - December 10, 2011
Habari ID: 2235470
Shirika La Kiislamu la Elimu Sayansi na Utamaduni ISESCO limetoa toleo jipya la jarida la lugha ya Kiingereza la Sayansi na Teknolojia.
Jarida hilo limechapishwa na Kituo cha Ustawishaji Utafiti wa Kisayansi la UNESCO.
Jarida hili la kila miaka miwili lina makala za wasomi na watafiti kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu. Makala hizo huchunguzwa na jopo la wataalamu kabla ya kuchapishwa. Jarida hilo lina makala kuhusu sayansi ya tiba, bioteknolojia, teknolojia ya mawasiliano, kemia, jiolojia, usimamizi wa vyanzo vya maji, sayansi za kilimo na kulinda mazingira.
Jarida la Sayansi na Teknolojia la ISESCO linalenga kustawisha mawasiliano baina ya wasomi na wataalamu wa teknolojia kutoka nchi wanachama na kuwaarifisha katika jamii ya kimataifa ya sayansi.
Toleo hilo jipya lina makala 12 za wasomi Waislamu kutoka Burkina Faso, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Bangladesh, Pakistan, Armenia, Indonesia, Japan, Cameroon na Uingereza.
912292
captcha