IQNA

Maonyesho ya nakala za hati za mkono za Kiislamu kufanyika Najaf

10:09 - December 11, 2011
Habari ID: 2236385
Mwenyekiti wa kamati ya uandishi vitabu, filamu za matukio ya kweli na uchapishaji ya mpango wa 'Najaf, Mji Mkuu wa Kiutamaduni wa Ulimwengu wa Kiislamu Mwaka 2012', amesema kuwa nakala elfu 4 za maandishi ya mkono ya Kiislamu na filamu za athari za kale zitaonyeshwa katika shughuli zinazohusiana na mpango huo.
Ali Marza amesema kuwa hifadhi, uchapishaji na kazi ya kutayarisha athari elfu nne za filamu, vitabu na nakala za maandishi ya mkono kuhusu historia ya kale na sasa ya mji mtakatifu wa Najaf nchini Iraq, imekamilika.
Amesema kuwa kazi hizo zitaonyeshwa kwa watu wote mwezi Machi mwakani kabla ya kuzinduliwa rasmi shughuli za mpango wa Najaf, Mji Mkuu wa Ulimwengu wa Kiislamu.
Ali Marza ameongeza kuwa wataalamu wa kamati hiyo pia wametayarisha insaiklopidia ya sayansi itakayoonyeshwa kwenye shughuli za mpango wa Najaf Mji Mkuu wa Kiutamaduni wa Ulimwengu wa Kiislamu mwaka 2012 ambayo ina habari kuhusu wana fasihi na wasomi wa elimu mbalimbali wa mji mtakatifu wa Najaf. 912974
captcha