Hizbullah imetoa taarifa ikiyataja matamshi hayo ya matusi ya mwanasiasa huyo wa Marekani, ambaye wakati mmoja alikuwa spika wa Congress ya Marekani kwamba ni ya kijahili na kipumbavu. Imesema matamshi hayo kwa upande mmoja yanabainisha wazi ujahili wa mwanasiasia huyo kuhusiana na historia ya kale na ya sasa ya Palestina na kwa upande wa pili yanabainisha juhudi zake za uadui na chuki kwa lengo la kupotosha ukweli wa kihistoria.
Hizbullah imesisitiza kwamba ulimwengu mzima unatambua vyema kwamba Wapalestina wamekuwa wakiishi kwa maelfu ya miaka katika ardhi zanazokaliwa sasa kwa mabavu na Wazayuni wa Israel na kwamba wana utamaduni na ustaarabu mkongwe ambao wamejitengenezea katika kipindi kirefu cha historia.
Harakati hiyo ya mapambano ya Kiislamu ya Lebanon imesisitiza kwamba matamshi kama hayo ya wanasiasa wa Marekani yanabainisha wazi siasa zao za ubaguzi, uadui na chuki dhidi ya taifa la Palestina, la sivyo hakuna mtu yoyote anayeweza kutaja mapambano halali ya taifa hilo dhulumiwa kuwa ni ugaidi.
Hizbullah imeashiria msimamo dhaifu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuhusiana na matamshi kama hayo ya chuki na ubaguzi dhidi ya taifa la Palestina na kuhoji kuwa je, mara hii itachukua hatua ya kukabiliana nayo au kama kawaida yake, itaendelea kukaa kimya mbele ya hujuma kubwa na hatari inayoendeshwa na maadui dhidi ya ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu?913236