Kwa niaba ya Mfalme wa Saudi Arabia, Gavana wa Mkoa wa Makkah mwanamfalme Khaled Al-Faisal ameongeza sherehe za kuisafisha Kaaba Tukufu siku ya Jumamosi kwa kutumia maji ya Zamzam yaliyochanganywa na maji ya waridi.
Hafla hiyo imehudhuriwa na idadi kubwa ya shakhsia wa ngazi za juu akiwemo Sheikh Saleh Al Hosain, Mkuu wa Idara ya Uongozi wa Haramain na Profesa Ekmeleddin Ihsanoglu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu.
Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Waziri wa Hija wa Saudi Arabia Fouad Al Farsi, Meya wa Makkah Osama Al Bar na Abdul Azizi Al Khodairy Naibu Gavana wa Makkah. Aidha wanadiplomasia wa nchi za Kiislamu na maafisa wa Msikiti Mkuu wa Makkah pia walidhuhuria hafla hiyo.
Eneo la ndani ya Al Kaaba huoshwa mara mbili kwa mwaka, katika mwezi wa Muharram na Shaaban, miezi ya kwanza na tisa katika kalenda ya Hijria.
Al Kaaba ndio nyumba ya kwanza iliyojengwa duniani kumuabudu Mungu Moja na inajulikana pia kama 'Baitul Ateeq" yaani nyumba ya kale zaidi. 913205