IQNA

Kongamano la 'Muhammad (saw): Mfano Mwema kwa Ulimwengu' lafanyika

11:16 - December 12, 2011
Habari ID: 2237093
Kongamano la Muhammad (saw): Mfano Mwema kwa Ulimwengu' umepangwa kufanyika Ijumaa ijayo huko katika mji wa Nantes nchini Ufaransa.
Kwa mujibu wa tovuti ya vds-nantes kongamano hilo linalodhaminiwa na Jumuiya ya Ijumaa za Mwamko lina lengo la kuarifisha sira na maisha ya Mtume Muhammad (saw) nchini Ufaransa.
Kufuatia kesi nyingi za magazeti ya Ufaransa kuchapisha makala yanayomvunjia heshima Mtukufu Mtume (saw) jumuiya za Kiislamu za Ufaransa zimekuwa zikifanya juhudi za kuandaa vikao mbalimbali vya kumuarifisha Mtume halisi wa Uislamu ili kwa njia hiyo kuweza kukabiliana na wimbi kubwa la hujuma inayofanywa na maadui dhidi ya mafundisho ya Kiislamu.
Jumuiya ya Ijumaa za Mwamko imetoa taarifa ikisema kuwa kuarifishwa vyema Mtume Mtukufu si tu kuwa ni jambo la dharura bali ni wajibu wa kila Mwislamu. Imeendelea kusema kuwa Waislamu wote pia wanawajibika kuchukua hatua za dharura kwa madhumuni ya kupambana na vitendo vya dharau na uvunjiwaji heshima Mtume Mtukufu (saw) pamoja na matukufu mengine ya Kiislamu.
taarifa hiyo imesema Waislamu wanapasa kujibu hadharani maswali mbalimbali yanayoulizwa na watu kuhusu dini ya Kiislamu na kufunga njia zote zinazotumiwa na maadui kuuhujumu Uislamu. 913397
captcha