IQNA

Kongamano la kimataifa la 'Qur'ani na Changamoto za Sasa' laanza Kufa

17:16 - December 13, 2011
Habari ID: 2238218
Kongamano la tatu la kimataifa la 'Qur'ani na Changamoto za Sasa' limeanza kazi zake katika mji wa Kufa nchini Iraq. Kongamano hilo linasimamiwa na kitengo cha malezi cha Chuo Kikuu cha Kufa.
Kongamano hilo linahudhuriwa na wasomi na watafiti kutoka nchi mbalimbali chini ya kaulimbiu ya "Izungumzisheni Qur'ani".
Miongoni mwa masuala yanayochunguzwa na wasomi wanaoshiriki katika kongamano hilo ni pamoja na 'uchunguzi wa tarjumi mbalimbali za Qur'ani Tukufu', 'Qur'ani na jamii, kuvumiliana, ugaidi, uadilifu, maadili na demokrasia', 'sheria za Qur'ani, haki za wachache na adhabu', 'Qur'ani Tukufu na elimu ya sasa', 'mipango ya kusambaza Qur'ani, kiraa na hifdhi ya kitabu hicho' na Qur'ani Tukufu, mwanamke, vazi la hijabu, haki na wajibu wa mume na mke'.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kufa alihutubia kikao cha kwanza cha kongamano hilo la kimataifa akisisitiza juu ya udharura wa kutaamali ndani ya Qur'ani, kuzidisha utafiti wa kitabu hicho na siri za utume wa Nabii Muhammad (saw) katika vyuo vya Kufa. 914390

captcha