Ali Akbar Velayati Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu amehutubia kikao cha waandishi habari mjini Tehran na kusema kuwa hatimaye vyombo vya habari vya Kimagharibi vimekiri kuhusu utambulisho wa Kiislamu wa mwamko wa watu katika eneo la Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika.
Kuhusu iwapo neno ‘Mwamko wa Kiislamu’ au ‘Machipuo ya Kiarabu’ litumiko kuarifisha utambulisho wa mwamko katika eneo maeneo hayo amesema, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika hotuba moja Machi 2011 alifafanua kuwa mwamko wa wananchi katika nchi za Kiarbau ni ‘Mwamko wa Kiislamu’ na hilo lilithibiti kutokana na yaliyojiri mashinani.
Wale wote wanaoshiriki katika maandamano katika nchi za maeneo hayo wamekuwa wakitoa nara za Kiislamu na maandamano makubwa kawaida hufanyika baada ya Sala ya Ijumaa, amesema Velayati ambaye wakati moja alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje Iran.
Amesema nchini Misri makundi ya Kiislamu hasa Ikwanul Muslimin yameshinda viti vingi bungeni na hili linaonyesha kufungamana wananchi na misingi ya Kiislamu. Velayati amedokeza kuwa Jumuiya ya Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu yenye makao yake hapa Tehran inapanga kuitisha kikao maalumu cha vijana, wanawake, waandishi na wasanii kutoka nchi za Kiislamu katika mustakabali wa karibu.
915049