Ofisi ya Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Husseini Sistani, mwanazuoni na mara'ja mashuhuri wa Kishia nchini Iraq imetoa taarifa ikikosoa vikali hatua ya dharau na uzushi iliyochukuliwa hivi karibuni na maadui kwa ajili ya kuchafua sura halisi ya Ushia duniani.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Nun, hivi karibuni baadhi ya tovuti zilizo na malengo maalumu dhidi ya Ushia zilichapisha sura bandia na za uongo mtupu zinazomwonyesha mwanazuoni huyo wa Kishia akiwa katika hali ya eti kujikatakata kwa upanga katika maombolezo ya Ashura.
Ofisi hiyo ilitoa taarifa hiyo hapo jana Jumanne ikikanusha vikali uzushi huo wa wazi dhidi ya mwanazuoni huyo wa Kishia anayeheshimika kitaifa na kimataifa.
Tarifa hiyo imesema kuwa ofisi iliyotajwa imesikitishwa mno na usambazwaji wa picha hizo za uongo na fitina na kusema kuwa bila shaka zimesambazwa na watu walio na malengo maalumu ya kiuadui dhidi ya madhehebu ya Kishia. 915204