IQNA

Mawaziri wa Utamaduni wa nchi za Kiislamu kukutana Algiers

15:57 - December 17, 2011
Habari ID: 2239121
Mkutano wa saba wa mawaziri wa utamaduni wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu utafanyika Jumapili ijayo katika mji mkuu wa Algeria , Algiers.
Kwa mujibu ripota wa IQNA tawi la Afrika, mkuano huo utafanyika chini ya anuani ya 'Kuimarisha Matokeo ya Mwaka wa Kimataifa wa Ukuruba wa Tamaduni'. Mkutano huo pia utajadili suala la uwezeshaji nafasi ya vijana katika kujenga utamaduni wa amani na mazungumzo.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Utamaduni ya Algeria imesema kongamano hilo la siku mbili pia litajadili suala la kuimarisha ushirikiano wa kiutamaduni baina ya nchi za Kiislamu.
Katika upande mwingine imearifiwa kuwa Mkutano wa 9 wa Mawaziri wa Habari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) umepangwa kufanyika Libreville, mji mkuu wa Gabon.
Katibu Mkuu wa OIC Ekmeleddin Ihsanoglu ameuambia ujumbe wa Gabon kwamba hii itakuwa mara ya kwanza kwa mkutano huo wa Mawaziri wa Habari wa nchi za Kiislamu kufanyika nchini humo.
915857
captcha