IQNA

Duru ya tano ya kikao cha Sanaa za Kiislamu kufanyika Kuwait

22:57 - December 19, 2011
Habari ID: 2241496
Duru ya tano ya kikao cha Sanaa za Kiislamu kimepangwa kufayika nchini Kuwait tarehe 25 Disemba. Kikao hicho kimeandaliwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Kuwait.
Kwa mujibu wa gazeti la al-Qabas la Kuwait, kikao hicho kitafanyika katika msikiti mkuu wa Kuwait kwa usimamizi wa Mohammad Al Afassi, Waziri wa Leba na Masuala ya Kijamii wa Kuwait pamoja na mwenzake wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu.
Kikao hicho ambacho kitahudhuriwa na mashirika pamoja na taasisi kadhaa za ndani na nje ya Kuwait kitafanyika katika msikiti uliotajwa ili kuonyesha nafasi muhimu ya msikiti katika jamii ya Kuwait.
Waandaaji wa kikao hicho wanasema kuwa wanafanya juhudi za kueneza utamaduni halisi wa Kiislamu na vilevile kuimarisha nafasi ya Kuwait katika kuunga mkono sanaa za Kiislamu. Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Kuwait mbali na shughuli za msikitini imekuwa ikijishughulisha pia na mambo mengine mengi kwa ajili ya kueneza utamaduni wa Kiislamu katika jamii ya nchi hiyo. 918376
captcha