'Ni juhudi za kujenga ustaarabu wa Kiislamu' amesema mwenyekiti wa ICMI Ilham Akbar Habibie.
Ameongeza kuwa mtandao wa kidijitali wa misikiti utahuisha nafasi iliyosahaulika ya kijamii ya misikiti katika umma. Aidha mpango huo utaimarisha jukumu la misikiti kama kituo cha elimu, afya na ushirika.
'Misikiti si eneo la kufanyia ibada tu', amesema.
Ilham amesema kuwa mpango huo utatimia intaneti kubuni mtandao wa mawasiliano miongoni mwa misikiti nchini Indonesia.
Kuna misikiti laki tisa nchini Indonesia ambayo imesajiliwa rasmi katika Baraza la Misikiti la nchi hiyo. Hata hivyo baadhi ya taarifa zinasema kuna misikiti mingine nusu milioni ambayo haijasajiliwa.
917631