IQNA

Katibu Mkuu wa OIC aonya juu ya tishio la Uzayuni huko Palestina

16:28 - December 20, 2011
Habari ID: 2241968
Akizungumza hivi karibuni katika kikao cha saba cha Mawaziri wa Utamaduni wa nchi za Kiislamu huko Algeria, Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) metahadharisha dhidi ya njama za utawala ghasibu wa Israel za kutaka kufuta utamaduni wa taifa la Palestina.
Katibu Mkuu huyo amesema kuwa mjadala wowote kuhusiana na masuala ya kiutamaduni ambao hautazingatia kwa njia maalumu masuala ya kutekwa ardhi za Wapalestina na utawala haramu wa Israel, hatari ya utawala huo kwa utamaduni wa Wapalestina kupitia uchimbaji wa njia za chini kwa chini katika Msikiti wa al-Aqsa na mashambulio ya kinyama ya utawala huo katika maeneo matakatifu kukiwemo kuchomwa moto misikiti na Qur'ani tukufu, hauwezi kuwa na natija yoyote ya kuridhisha.
Ihsanoglu amezungumzia umuhimu wa Quds Tukufu na maeneo mengine matakatifu katika ardhi za Wapalestina kwa ulimwengu wa Kiislamu na Kikristo na kusisitiza kwamba kuenedelea siasa za uharibifu na zinazokwenda kinyume na sheria za kimataifa za utawala haramu wa Israel, ambazo ni pamoja na kuwafukuzwa Wapalestina katika ardhi na nyumba zao, hatua ya kujenga ukuta wa kibaguzi kwa ajili ya kuwatenga Wapalestina na kuyahudisha maeneo ya kihistoria ya Waislamu na Waarabu ni jambo linalolaaniwa vikali na ulimwengu wa Kiislamu.
Katibu Mkuu wa OIC ametahadharisha juu ya hatari ya utawala wa Kizayuni kuendelea kuchimba mashimo na njia za chini kwa chini katika Msikiti wa al-Aqsa na kuitaka jamii ya kimataifa na hasa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kutekeleza vilivyo majukumu yake na kuulazimisha utawala huo uheshimu sheria za kimataifa na kusimamisha mara moja uharibifu huo unaoufanya huko Quds.
Ihsanoglu pia ameashiria siasa za chuki zinazoenezwa dhidi ya Uislamu barani Ulaya na Marekani na kutaka hatua madhubuti zichukuliwe kwa lengo la kuarifisha sura halisi ya Uislamu katika nchi za Magharibi ili kukabiliana na njama zinazoenezwa na vyombo vya habari vya nchi hizo dhidi ya Uislamu. 918826
captcha