IQNA

Walowezi wa Kizayuni wamvunjia heshima Mtume Muhammad (saw)

17:42 - December 20, 2011
Habari ID: 2242318
Walowezi wa Kizayuni wa Israel wamevamia Msikiti wa Sahaba katika mji wa Bani Naeem katika Ukingo wa Magharibi huko Palestina na kuandika maneno yanayomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) katika kuta za msikiti huo.
Imamu wa Msikiti wa Sahaba Jihad Munasira amesema kuwa walowezi wa Kiyahudi mapema jana walishambulia msikiti huo ulioko mashariki mwa al Khalil na kuandika nara za kibaguzi dhidi ya Waislamu katika mlango wake. Wazayuni hao walivunja mlango na kuingia ndani ya msikiti huo ambako wameandika maneno yanayomvunjia heshima Mtume wa Uislamu katika kuta zake.
Jihad Munasira ameongeza kuwa baada ya kushuhudia maandishi hayo ya kejeli yaliyoandikwa kwa lugha ya Kiebrania ameripoti uvamizi huo kwa viongozi husika.
Katika wiki za hivi karibuni walowezi wa Kiyahudi wamekuwa wakivamia misikiti na maeneo matukufu ya Kiislamu na kushambulia wananchi wa Palestina na milki zao. Hadi sasa makumi ya misikiti na maeneo ya ibada ya Waislamu yamechomwa moto na walowezi hao wa Kizayuni. 919160
captcha