IQNA

Kongamano la ‘Nafasi Mpya ya Wanawake katika Ulimwengu wa Kiislamu’

15:19 - December 21, 2011
Habari ID: 2242735
Kongamano la Kimataifa lenye anwani ya ‘Nafasi ya Wanawake katika Jamii ya Kiislamu inayobadilika’ linafanyika Disemba 21-25 huko Istanbul Uturuki chini ya usimamizi wa Muungano wa Kibunge wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na Wizara ya Familia na Sera za Jamii ya Uturuki.
Kongamano hilo linatarajiwa kufunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Kongamano hilo litajadili uzoefu wa kitaifa katika kuunda mfumo wa usawa wa kijinsia, kushirikishwa wanawake katika siasa, uimarishwaji demokrasia, haki za wanawake Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika, Uislamu na Demokrasia na uanzishwaji taasisi za kutetea haki za wanawake.
919452
captcha