IQNA

Warsha kuhusu shule za Kiislamu-Kiarabu Mali

14:01 - December 24, 2011
Habari ID: 2243564
Shirika la Kiislamu la Elimu Sayansi na Utamaduni ISESCO limepanga warsha kuhusu ustawi wa shule za Kiislamu-Kiarabu huko Bamako mji mkuu wa Mali kuanzia 26-29 Disemba.
Warsha hiyo itawakutanisha pamoja wakuu 20 wa shule za Kiislamu-Kiarabu kutoka Algeria, Tunisia, Senegal, Guinea, Guinea Bissau, Burkina Faso, Morocco, Mauritania na Mali.
Warsha hiyo inalenga kuimarisha shule za Kiislamu Kiarabu kwa kuangazia matatizo ya kiakademiki, kielimu, kifedha na mfumo wa usimamizi.
Washiriki pia watachunguza njia za kivitendo za kuimarisha kiwango cha elimu katika shule hizo pamoja na kuzijumuisha na shule za kawaida zisizo za kidini.
Vilevile washiriki watabadilishana mawazo na uzoefu kuhusu shule za Kiislamu-Kiarabu na kuangazia mustakabali wa shule hizo.
Youssef Abou Daka wa ISESCO ambaye ni mtaalamu wa masuala ya elimu atasimamia warsha hiyo.
920276
captcha