IQNA

Mufti wa Syria asisitiza kulindwa umoja wa ndani

10:39 - December 26, 2011
Habari ID: 2245257
Mufti wa Syria ametoa taarifa kufuatia milipuko ya kigaidi iliyotokea nchini humo hivi karibuni akisisitiza juu ya ulazima wa kulindwa umoja wa kitaifa kwa lengo la kupambana na njama za Marekani na utawala haramu wa Israel dhidi ya nchi hiyo.
Amewataka Wasyria kuswali katika misikiti ya nchi hiyo ili kufariji nyoyo za mashahidi waliouawa katika milipuko ya kigaidi ya hivi karibuni mjini Damascus.
Sheikh Ahmad Badru Deen Hassun, amesisitiza kwamba matukio yanayoendelea sasa nchini Syria yanawalazimu Wasyria kusimama imara katika safu moja kwa lengo la kukabiliana na hujuma ya wageni dhidi ya nchi hiyo. Amesema ni wazi kuwa matukio hayo yanatokana na uchokozi wa moja kwa moja wa Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Taifa la Syria, uchokozi ambao amesema kwa bahati mbaya unaungwa mkono na baadhi ya wahaini na wasaliti nchini humo.
Amesema kila mtu ambaye leo hii amekaa kimya na kudai kwamba hapendelei upande wowote katika mgogoro huo, kwa hakika atakuwa amechukua msimamo dhidi ya maslahi ya taifa lake.
Wanazuoni wengine wa Syria pia wametoa taarifa tofauti wakiwataka Wasyria kuwa waangalifu kuhusu njama za wageni dhidi ya nchi yao. Wamesisitiza kuwa wataendelea kushirikiana na wananchi katika kupambana na ugaidi na vitendo vya mabavu ambavyo havina uhusiano wowote na mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu.
Mazishi ya mashahidi 44 wa mashambulio hayo ya kigaidi ambayo pia yalipelekea watu wengine 166 kujeruhiwa, yalifanyika Jumamosi iliyopita mjini Damscus. 922164
captcha