Sheikh wa al Azhar ameyasema hayo baada ya viongozi wa makundi mbalimbali ya Palestina kukutana mjini Cairo na kufikia mapatano muhimu. Amewataka Wapalestina wote kulinda umoja na mshikamano wao katika kuelekea kwenye suluhu ya kitaifa.
Sheikh Tayyib amesisitiza kuwa makundi yote ya Palestina yanapaswa kujiepusha na hitilafu na mifarakano kwa ajili ya kupambana na utawala ghasibu wa Israel na kukabiliana na mipango ya utawala huo ya kuiyahudisha Quds Tukufu.
Vilevile amezitaka jumuiya ya taasisi za Kiislamu kuwasaidia na kuwaunga mkono Wapalestina katika juhudi zao za kupambana na njama za utawala ghasibu wa Israel kwani wajibu mkubwa zaidi wa umma wa Kiislamu katika kipindi cha sasa ni kulinda Msikiti wa al Aqsa na Quds Tukufu.
Sheikh wa al Azhar amesisitiza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel hauna haki yoyote katika wakfu za Kiislamu za Quds Tukufu na Wapalestina ndio wenye mamlaka kwenye wakfu hizo. 922690