"Nchi zilizofanikiwa zimeweza kufanya hivyo kwa sababu wanawake walisimama bega kwa bega na wanaume" alisema huku akisifu nafasi ya wanawake katika kuleta mabadiliko ya kijamii na kisiasa katika nchi za Mashariki ya Kati.
Katika taarifa yake kwa kikao cha kimataifa cha siku ya Ijumaa kuhusu 'Mabadiliko katika Jamii za Waislamu na Nafasi ya Wanawake', Ihsanoglu amesisitiza kuwa ni kupitia kuongeza ushiriki wa wanawake katika nyuga za kisiasa na kijamii ndio mataifa yatapiga hatua imara za maendeleo.
Aidha amezungumzia juhudi za OIC za kuimarisha nafasi ya wanawake katika nchi 57 wanachama. Amesema moja ya juhudi hizo ni kongamano la kwanza la mawaziri kuhusu nafasi ya wanawake Waislamu. Kongamano hilo lilifanyika hivi karibuni mjini Istanbul Uturuki.
921950