IQNA

Mwamko wa Kiislamu wafuta fikra za utaifa wa Kiarabu

14:06 - December 27, 2011
Habari ID: 2245867
Mwanasiasa mmoja wa Iran amesema wimbi la mwamko wa Kiislamu litafuta fikra za ukereketwa wa utaifa wa Kiarabu na fikra zingine za kibaguzi.
Hamid Reza Taraqi mkuu wa masuala ya kimataifa katika Chama cha Muungano wa Kiislamu amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa wimbi hilo la mwamko litaufanya Uislamu kuwa mhimili mkuu wa umoja miongoni mwa Waislamu duniani.
Ameongeza kuwa mwamko wa Kiislamu Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika umeonyesha kuwa Waislamu wako tayari kuwa na umoja na mshikamano. 'Aidha mwamko huu umeyakumbusha mataifa kuhusu uwezo wa ulimwengu wa Kiislamu kuwa mjumuiko wenye nguvu duniani'.
Kuhusu fikra ya kuanzishwa muungano wa nchi za Kiislamu, amesema ulimwengu wa Kiislamu unapaswa kuwa na mkakati wa kujihami mbele ya hujuma za maadui na kuzuia dhulma katika nchi za Kiislamu.
Amesisitiza kuwa demokrasia ya kidini inapaswa kuhimizwa hasa katika kipindi hiki ambapo serikali mpya zimekuja madarakani kufuatia mwamko wa Kiislamu.
922767
captcha