Gazeti hilo limesema kwamba Mayahudi wengi wamekuwa wakiathirika na vipindi vya Kiislamu ambavyo huwafikia kupitia mitandao ya intaneti na televisheni za satalaiti zinazorusha hewani vipindi vyao kutokea Mashariki ya Kati na Ulaya.
Abu Hassun, mhubiri wa Kiislamu amesema kuhusiana na suala hilo kwamba kutokana na kutokuwepo wahubiri wa kutosha wa Kiislamu huko Israel, yeye na wenzake wameanzisha jumuiya ya ar-Rahma kwa lengo la kuwatayarishia Waislamu wapya wa Kiyahudi, vijitabu vya Kiislamu kwa lugha ya Kiibrania.
Gazeti la Ahronot limeendelea kusema kuwa Wizara ya Sheria ya utawala wa Kizayuni hadi sasa haijatayarisha ripoti kamili kuhusiana na Mayahudi wanaosilimu kati ya Mayahudi 600 ambao kila mwaka hubadili dini na imani yao. 923555