IQNA

Wakristo, sehemu muhimu ya jamii ya Iraq

15:33 - December 28, 2011
Habari ID: 2247090
Sayyid Ammar Hakim, Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq amesema katika ujumbe wake wa pongezi kwa Papa Benedict XVI, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, kwa mnasaba wa kuzaliwa Nabii Isa Masih (as) kwamba Wakristo wa Iraq wanaunda sehemu muhimu ya jamii ya nchi hiyo.
Sayyid Hakim amesema katika ujumbe huo kwamba kutokana na ukweli huo serikali imekuwa ikifanya kila iwezalo kutetea haki zao. Amesema serikali ya Iraq haiwabagui raia wa nchi hiyo kwa msingi wa kidini na kwamba inafanya kila iwezalo kutetea haki na maslahi ya kila mwananchi.
Sayyid Hakim ameyataka mataifa tofauti ya dunia kufanya jitihada za kuimarisha amani na mazingira ya kuishi pamoja kwa amani na ushirikiano wafuasi wa dini tofauti.
Vilevile amekumbusha mwishoni mwa ujumbe wake huo juu ya umuhimu wa wafuasi wa dini za mbinguni kufuata mafundisho ya mitume na manabii wa Mwenyezi Mungu kwa kuishi pamoja kwa amani na kuheshimiana na wakati huohuo kulinda na kutetea damu ya mwanadamu. 924327
captcha