IQNA

Chuo Kikuu cha Michigan kuchunguza historia ya Waislamu nchini Marekani

15:31 - December 28, 2011
Habari ID: 2247108
Kwa mara ya kwanza somo jipya la 'Historia ya Waislamu nchini Marekani' limepangwa kutolewa katika Chuo Kikuu cha Michigan nchini Marekani.
Kwa mujibu wa Islam Today, viongozi wa chuo hicho wamechukua uamuzi wa kuanzisha somo hilo kutokana na ombi la wanachuo walio na hamu ya kusoma na kutalii masuala ya Kiislamu na Marekani na vilevile Kiarabu na Marekani. Masomo hayo yanatazamiwa kuanza katika chuo kilichotajwa katika msimu huu wa baridi.
Wiki iliyopita viongozi wa Chuo cha Sanaa na Sayansi cha Chuo Kikuu cha Michigan pia walipendekeza kuanzishwa kitengo kipya cha Utafiti wa Kiarabu na Marekani, pendekezo ambalo lingali linajadiliwa na wakuu husika.
Wanaopigania kuanzishwa kwa kitengo hicho kipya cha masomo wanasema kuwa kitawasaidia wanachuo kuwa na ufahamu wa kitosha kuhusiana na hali ya Waislamu wa Marekani pamoja na historia ya kuingia Uislamu nchini humo. 924441
captcha