Waziri Mkuu wa Serikali halali ya Palestina Ismail Hania aliwasili jana mjini Khartoum akiongoza ujumbe wa Palestina unaoshiriki katika kongamano hilo.
Ismail Hania amewaambia waandishi habari katika uwanja wa ndege wa Khartoum kwamba ameenda nchini Sudan kushiriki kwenye kongamano hilo la kimataifa kwa shabaha ya kukabiliana na siasa za kupenda kujitanua za utawala haramu wa Israel na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina.
Waziri Mkuu wa serikali iliyochaguliwa na wananchi ya Palestina amesema kongamano hilo la Khartoum ni hatua muhimu ya kukabiliana na siasa za utawala wa Kizayuni wa Israel na sisitizo la nafasi ya Kiislamu, Kiarabu na Kipalestina ya Quds Tukufu na ameishukuru serikali ya Sudan kwa kutayarisha kongamano hilo.
Ismail Hania amesisitiza juu ya udharura wa kulindwa haki za umma wa Kiislamu na akasema Hamas haitafumbia jicho hata shibiri moja ya ardhi ya Palestina na wala haitawaruhusu wavamizi wa Kizayuni kuitwaa Quds Tukufu. 924787