IQNA

Kesi ya dikteta Mubarak yaakhirishwa tena

17:20 - December 29, 2011
Habari ID: 2247522
Kwa mara nyingine tena watawala wa kijeshi wa Misri wameakhirisha kesi ya dikteta Hosni Mubarak aliyeng'olewa madarakani hivi karibuni nchini Misri na kusema kuwa itafanyika tarehe Pili Januari mwakani.
Kesi hiyo ilitazamiwa kuendeshwa leo mjini Cairo dhidi ya Hosni Mubarak pamoja na wanawe wawili, wasaidizi wake sita pamoja na Habib al-Adli, Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani anayetuhumiwa kuhusika na ubadhirifu wa fedha za umma pamoja na kuwaua Wamisri walioshiriki katika maandamano ya 25 Februari.
Mahakama ya Jinai ya Cairo imeakhirisha mara kadhaa kesi dhidi ya wahalifu hao, na sasa inadai kwamba itaendelea siku ya Jumatatu ijayo. Mahakama hiyo ambayo inasimamiwa na Ahmad Raf'at imepokea ripoti kuhusiana na uchunguzi uliofanyika kuhusu kesi inayowakabili watuhumiwa waliotajwa na imewapa fursa ya kujitetea mahakamani. 924875
captcha