IQNA

Haniya aonya dhidi ya njama za Israel za kuyahudisha Quds

15:15 - December 31, 2011
Habari ID: 2248257
Akizungumza hapo jana Ijumaa katika Msikiti wa an-Nur mjini Khartoum, mji mkuu wa Sudan, Ismail Haniya, Waziri Mkuu wa serikali halali ya Palestina ametahadharisha dhidi ya njama za utawala haramu wa Israel za kutaka kuufanya mji wa Quds kuwa wa Kiyahudi na kusisitiza kuwa mji huo mtakatifu unakabiliwa na hatari kubwa kutoka kwa Wazayuni.
Haniya amesema kuwa uchokozi wa mara kwa mara wa Israel katika ardhi za Wapalestina na hasa katika Ukanda wa Gaza unahitaji kukabiliwa na jibu la wazi na thabiti ili kuzuia kuenezwa kwa siasa na njama haribifu za utawala huo huko Quds, Masjidul Aqsa na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Ismail Haniya ameendelea kusema kwamba utawala haramu wa Israel umekuwa ukijenga vitongoji vipya vya Mayahudi na kuharibu athari na nembo za Kiarabu na Kiislamu huko Quds na vilevile Masjidul Aqsa, yote hayo ikiwa ni katika juhudi za utawala huo ghasibu za kuitenga Quds na ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu.
Waziri Mkuu wa Palestina amesisiza kwamba hii leo Quds inahitaji mambo mawili muhimu la kwanza ni uungaji mkono mkubwa wa kifedha kwa mapambano ya Wapalestina, wakazi na taasisi za Quds na la pili ni uungaji mkono thabiti wa kisiasa kwa Quds katika duru za kimataifa. 925806
captcha