Amesisitiza kuwa, "kutafuta elimu kwa maana yake ya kina" na "kueneza fikra sahihi pamoja na kutangaza misimamo halisi ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu" ni miongoni mwa majukumu makuu ya wanachuo hao.
Aidha ametoa ufafanuzi kuhusu jukumu kuu la wanafunzi hao yaani kutafuta elimu na kukumbusha kuwa, kukosekana uwezo na nguvu za kielimu na kimaanawi ndilo lililokuwa tatizo kubwa nchini Iran kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu na jambo hilo liliandaa mazingira ya taifa la Iran kuwa tegemezi kwa madola ya kigeni.
Ameongeza kuwa, ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na moyo wenye sifa ya kipekee aliokuwa nao Imam Khomeini (quddisa sirruh) katika kutawakali na kumtegemea Mwenyezi Mungu na kuliamini taifa, kuliandaa mazingira ya kupatikana moyo wa kujiamini kitaifa nchini Iran na kulifanya taifa hili lifanikiwe kutoka katika minyororo ya kuzingirwa kiroho na sasa taifa la Iran linajitatulia lenyewe mambo yake.
Ayatullah Udhma Khamenei ametoa ufafanuzi pia juu ya kazi ya pili kuu ya wanachuo wa Iran walioko nje ya nchi nayo ni kueneza fikra sahihi na kubainisha kwa njia bora misimamo halisi ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu katika kukabiliana na maadui.
Ameonge za kuwa, Iran ya Kiislamu imepata mafanikio makubwa sana katika kukabiliana na ubeberu na kanali tata sana na adhimu ya kiuchumi na kipropaganda ya maadui hao, ambapo kuweza kukabiliana na vikwazo vingi dhidi yake na kupiga hatua za maendeleo katika kadhia ya nyuklia ni sehemu moja tu ya matunda na mafanikio hayo. Amesema, hali hii ya ushindi wa Iran ya Kiislamu Inshaallah itaendelea.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza pia juu ya udharura wa kufanyika jitihada kubwa zaidi ili kuimarisha nukta chanya na uwezo wa kielimu katika njia hiyo na kukumbusha kuwa: Adui anachukua hatua kubwa sana za kisiasa, kiusalama na kiuchumi katika mambo yote dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, lakini pamoja na hayo hivi sasa misingi ya adui huyo inalegalega na anazidi kushindwa na kufeli.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Hujjatul Islam Walmuslimin Ejei, mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Umoja wa Jumuiya ya Kiislamu ya Wanachuo wa Ulaya ameashiria kikao kikuu cha 46 cha umoja huo na kutoa ripoti kuhusu matunda na mafanikio ya umoja huo katika nyanja mbali mbali za kielimu na utafiti.
926851