IQNA

Taasisi ya utafiti wa bidhaa halali kuanzishwa Iran

15:45 - January 04, 2012
Habari ID: 2250969
Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeidhinisha mpango wa kuanzishwa Taasisi ya Utafiti wa Bidhaa Halali kwa lengo la kuchunguza uhalali wa bidhaa zinazoingizwa humo nchini.
Kwa mujibu wa IQNA, Ahmad Sheibani Mkuu wa Shirika la Vyakula na Madawa la Iran amesema taasisi hiyo itajumuisha kamati ya maafisa wa shirika hilo, maafisa wa kibiashara na vilevile mwakilishi wa Wizara ya Afya.
‘Kamati hii itachunguza bidhaa za vyakula, kitiba n.k zinazoingizwa Iran kwa lengo la kuwahakikishia wananchi kuhusu uhalali wa kidini wa bidhaa hizo’, amesema.
Kumeshuhudiwa ustawi mkubwa wa mashirika yanayozalisha bidhaa halali duniani hasa vyakula. Hata hivyo bado kuna wasi wasi kuwa baadhi ya mashirika hayo yamkini yakauza bidhaa zisizo halali lakini zikwa na nembo ya ‘Halal’.
927423
captcha