Bomu hilo la moto lilirushwa ndani ya Msikiti wa Kituo cha Kiislamu cha Imam Al Khoei wakati Waislamu 80 wakiwa ndani.
Hakuna ripoti za majeruhi katika tukio hilo. Aidha nyumba mbili karibu na sehemu hiyo zililengwa na magaidi hao walioushambulia msikiti.
CAIR imetaka taasisi za Kiislamu na polisi kuchukua hatua za kuimarisha usalama misikitini.
‘Hujuma dhidi ya nyumba za ibada inapaswa kulaaniwa na Wamarekani wote na uchunguzi ufanyike kwa lengo la kuwashtaki wahusika’, amesema Ibrahim Hooper, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano CAIR.
Ametaka Shirika la Upelelezi Marekani FBI kuchunguza kwa kina hujuma zinazofanywa dhidi ya misikiti na vitendo vingine vya chuki dhidi ya Uislamu.
Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kumeshuhudiwa hujuma dhidi ya misikiti katika maeneo kama vile Massachusetts, Oregon, Ohio, New York, Iowa, Maine, Georgia, Missouri, Louisiana, Tennessee, Texas, California, na Michigan.
928148