Huku akibainisha mgogoro mkubwa wa kiafya unaowakabili wagonjwa wa saratani na uhaba wa suhula za kuwatibu watu wenye matatizo ya figo, Ihsanoglu ameziomba nchi wanachama wa OIC pamoja na mashirika ya misaada ya kibinadamu kufanya juhudi za kuwasaidia wakazi wa Ukanda wa Gaza.
Ofisi za OIC mjini Gaza na Cairo zimetangaza kuwa ziko tayari kufanya utaratibu wa kutumwa misaada hiyo katika ukanda huo.
Uhaba wa suhula za tiba na madawa ya magonjwa sugu unahatarisha maisha ya wagonjwa wengi wa ukanda huo na hata upasuaji wa magonjwa ya macho, watoto na moyo umesimama kabisa. 928744