Kufuatia malalamiko ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Makerere cha Uganda dhidi ya kuzuiwa wanafunzi wa kike wenye vazi la hijabu kuingia kwenye vikao vya mtihani, idara ya uongozi wa chuo hicho sasa imewahakikishia Waislamu kwamba suala hilo halitakariri tena.
Tovuti ya Islam Today imeripoti kuwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Makerere umewaruhusu wanafunzi wa kike wa Kiislamu kuingia kwenye vikao vya mitihani wakiwa na vazi la hijabu kwa sharti kwamba wakubali kusachiwa kabla ya kuingia kwenye mtihani.
Uamuzi huo umechukuliwa baada ya malalamiko ya wanachuo Waislamu chuoni hapo dhidi ya sheria ya kuwazuia wanafunzi wa kike wenye vazi la hijabu kuingia kwenye vikao vya mitihani.
Wanafunzi hao wa Kiislamu wamesisitiza kuwa Chuo Kikuu cha Makerere kinapaswa kutumia wakaguzi wa kike katika kuwapekua wanafunzi wa kike wenye vazi la hijabu ya Kiislamu.
Wanafunzi Waislamu wa Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda wanasema tatizo lao kubwa ni kutokuwepo Waislamu katika baraza la uongozi wa chuo hicho na kwamba suala hilo linapelekea kuchukuliwa maamuzi yanayopuuza haki za wanachuo Waislamu. 928542